Ijue Smart EFD

Smart EFD ni bidhaa suluhishi ambayo imechunguza changamoto za EFD za kawaida, kubaini mapengo kati ya kile washindani wanachotoa na kile walipa kodi wanahitaji.

Mfumo wa risiti za EFD

Imetengenezwa kutoa na kutuma risiti kwa wateja kama nakala ngumu na laini kupitia barua pepe, Bluetooth, mitandao ya kijamii, ujumbe wa maandishi, na / au uchapishaji. Uchapishaji unahitaji kifaa kingine ambacho ni printa yenye uwezo wa Bluetooth inayounganishwa na simu ya mkononi.

Pia, unaweza kutoa risiti za anakra yaani Tax Invoice kwa wateja kama ilivyo risiti za EFD ikiwa ina kipengele cha nambari na picha ya QR kwaajili ya uthibitisho

Image
Image

Faida Kibiashara

Kutokana na kuunganishwa na mfumo wa TRA, ripoti zinatengenezwa kiotomatiki (Z Report) na kutumwa moja kwa moja kwenye mtandao za TRA. Nakala zilizotumwa za ripoti (X Report) zinahifadhiwa kwenye akaunti ya mteja na zinapatikana kwa urahisi wakati wowote. Kwa biashara zilizosajiliwa kwa VAT, wanaweza kudai kodi ya pembejeo (input tax).

Wamiliki wa biashara wana chaguo la kuomba akaunti zaidi ya moja kwa ajili ya vitengo vyao vya biashara vingine. Kupitia kipengele cha Msimamizi (Admin), wanaweza kudhibiti na kusimamia biashara zao kwa kuangalia ripoti za mauzo, kufuta akaunti, kuweka kiwango cha juu cha bei kwa kutoa risiti n.k.

Image

Uunganishaji wa Nje(Intergration)

Mfumo umewekwa kwa ajili ya kupokea maombi kupitia programu maalumu, na kuyashughulikia maombi hayo. Wateja wanaomiliki programu za kompyuta kama vile za mauzo na uhasibu wanaweza kuingiliana na Smart EFD.

Utunzaji wa Taarifa

Tumechukua hatua za usalama wa data na faragha kupitia mbinu za kuhifadhi kwenye wingu (cloud), na kuhakikisha usalama wa kutoa huduma za kompyuta ikiwa ni pamoja na seva, uhifadhi wa data, database, programu, n.k. kwenye majukwaa ya mtandaoni.

Image

Pakua app yetu kwenye simu janja yako